Top Stories

GOOD NEWS: Wenye matatizo ya moyo, kuna hii yakufahamu

on

Taasisi ya Jakaya Kikwete inayojihusisha na kutibu maradhi ya moyo JKCI imepata ugeni kutoka nchini India na imeanza kuanza kutoa mafunzo ya kutibu maradhi mbalimbali ya moyo kwa madaktari nchini ili kuboresha upatikanaji wa matibabu hayo na kupunguza watu kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge ameeleza kuwa wataalamu wa afya wamepokea mafunzo hayo kutoka kwa madaktari bingwa kutoka India ili kuweza kuanza kutoa huduma za matibabu ya moyo nchini na haya ni mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya na serikali kwani itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za matibabu ya moyo.

“Na kwa mafanikio haya taasisi hii ya moyo sasa itaweza kuanza kufanya pia upasuaji wa moyo kwa watoto wadogo hata wa umri wa mwezi mmoja.” – Dr Peter Kisenge

Ulipitwa na hii? Matibabu bure sio Ubungo tu, imewafikia na Wazee Kagera

Hii je? Mpango mwingine wa Ubalozi wa Marekani kwa wanafunzi TZ

Soma na hizi

Tupia Comments