Vituo vingi vya mafuta vimefungwa baada ya ukaguzi unaoendelea ambao unafanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ kuangalia kama vinafuata sheria na taratibu za kutumia mashine za kutolea risiti za kielektroniki maarufu kama EFPP zilizofungwa moja kwa moja kwenye pampu.
Unaambiwa vituo vya mafuta ambavyo havifuati sheria na taratibu kama walivyotakiwa kufanya vinafungiwa ambapo hadi sasa zoezi hilo limeonesha kuwagharimu wamiliki wake baada ya vituo kufungwa.
millardayo.com imetembelea kwenye vituo hivyo na kufanikiwa kuzinasa picha hizi katika baadhi ya vituo maarufu vya mafuta katika maeneo ya Sinza na Mwenge DSM.
Mtanzania aliyewahi kuweka rehani gari lake kumsadia kijana ada ya Shule…bonyeza PLAY kwenye VIDEO hii kutazama!!!