Top Stories

Utafiti: Wanawake wanashauriwa kulala zaidi ya wanaume….sababu?

on

Utafiti mpya uliofanywa Uingereza na kituo cha utafiti cha Chuo Kikuu cha Loughborough umeonesha kuwa wanawake wanahitaji muda mwingi zaidi wa kulala kuliko wanaume kwasababu kibailojia wanawake wana uwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na hilo hutumia nguvu nyingi ya ubongo.

Kutumika kwa nishati hii nyingi ya ubongo kunasababisha ubongo kuhitaji muda mwingi wa kupumzishwa ili kukarabati na kurejesha kwenye hali ya kawaida hususani sehemu ya kumbukumbu, lugha na nyinginezo.

Imeelezwa pia kuwa jinsi mtu anavyofanya kazi nyingi wakati wa mchana ubongo hua unahitaji muda mwingi zaidi wa kupumzika, tofauti na hapo matatizo ya kiafya hutokea ikiwemo ya kisaikoloji kama msongo wa mawazo, hasira na mengineyo.

Ulipitwa na hii? Barabara yafungwa, Polisi wasimamia jengo la Madaraka Mwanza likibomolewa

Hii je? Nyumba nyingine zaidi ya 100 zateketezwa Kagera

 

Soma na hizi

Tupia Comments