Premier Bet
TMDA Ad

AyoTV

KMC imepata dili la Tsh Bilioni 1 kwa miaka mitano, jezi mpya za 2019/20

on

Baada ya kufanya maajabu katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara wa 2018/19 na kumaliza nafasi ya nne ambayo imeisaidia kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika katika msimu wa 2019/2020, leo limetangazwa dili jipya la KMC.

KMC imefanikiwa kupata udhamini kutoka kampuni ya ubashiri ya M Bet wa miaka mitano wenye thamani ya Tsh Bilioni 1, mkataba walioingia KMC na M Bet unaeleza kuwa kutakuwa na awamu kadhaa za utolewaji wa pesa hizo lengo likiwa ni kuisaidia timu ili hata mabadiliko ya viongozi yakipita timu iweze kusimama.

Mkataba wa KMC na M Bet umesainiwa na Alen Mushi kwa upande wa M Bet na Mstahiki meya kwa upande wa KMC Benjamin Sitta, KMC kwa sasa inaelekea katika mchezo muhimu wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la shirikisho Afrika.

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments