Ikiwa ni takribani mwezi mmoja na siku kadhaa zimebakia kwa Barack Obama kumaliza kipindi cha cha utawala wa miaka nane akiwa Rais wa Marekani, tayari imejulikana sehemu atakayokwenda kuishi yeye na familia yake baada ya kustaafu.
Nimezipata picha za muonekano wa ndani ya nyumba hiyo inayotajwa kuwa na gharama ya dola za Marekani milioni 5.3 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania bilioni 11 iliyopo jijini Washington DC.
Pamoja na ukubwa ulioizidi nyumba ya Rais mteule wa nchi hiyo Donald Trump, bado haijaifikia gharama zake wala nyumba ya Rais yeyote aliyewahi kutawala Marekani.
Nyumba ya Obama ilijengwa mwaka 1928, kwenye eneo la ukubwa wa futi 8,200 huku ikiwa na vyumba 9 vya kulala.
Nimekuwekea hapa picha za muonekano wa nyumba hiyo
VIDEO: Huenda haufahamu kuhusu gharama zilizotumika kwenye malipo ya nyumba aliyoinunua Diamond Platnumz kwaajili ya familia yake Afrika Kusini. Tazama hapa.