Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Jamii FORUMS Maxence Melo amefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam December 16 2016 kwa mara ya kwanza toka akamatwe na Polisi ambapo alisomewa mashtaka yote yanayomkabili.
Wakili wake Jebra Kambole amesema mashtaka ya Max ni manne ambapo matatu yanafanana (kuzuia Polisi kufanya kazi yao) na shitaka la nne ni kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa Tanzania (.co.tz)
Baada ya kusomewa mashtaka mshitakiwa aliyakana na upande wa Jamhuri ukasema hauna pingamizi ambapo hata hivyo imeelezwa Max alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo akarudishwa Rumande.
AyoTVMAGAZETI: Prof. Ndalichako ageuziwa kibao, Siri nzito maiti saba mto Ruvu, Bonyeza play hapa chini