Mix

Full time ya Brazil vs Croatia. Matokeo na wafungaji haya hapa

on

Hatimaye baada ya subira ya miaka minne, wapenzi wa soka ulimwenguni kote leo wamepata ladha ya fainali za michuano ya kombe la dunia.

Mchezo wa ufunguzi ulichezwa leo baina ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia, matokeo ni 3-1, Brazil wakianza vizuri michuano hiyo mbele ya Croatia.

Magoli ya Brazil yamefungwa na Neymar, aliyefunga mawili, Oscar nae ambaye leo alikuwa kwenye kiwango bora aliongeza la 3.
Croatia wenyewe walianza kuziona nyavu zao kwenye mchezo huo walipata goli lao mapema kabisa ya mchezo baaada ya beki wa Brazil Marcelo kujifunga akiwa kwenye harakati za kuokoa.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho saa 1 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Mexico dhidi ya wawakilishi wa Afrika Cameroon.

20140613-010343-3823241.jpg

Tupia Comments