Michezo

Full time ya Real Madrid vs A.Bilbao na msimamo wa La Liga baada ya mechi za leo

on

Wakiwa hawajapoteza mchezo wowote tangu msimu ulipoanza wala kuruhusu goli hata moja kwenye ligi kuu ya Hispani – Real Madrid leo wamejitupa uwanjani kucheza dhidi ya Athletic Bilbao.

  
Wakicheza ugenini, Madrid wameendelea na rekodi yao ya kutofungwa baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Bilbao.

  
Karim Benzema baada ya kuipa ushindi Madrid mechi iliyopita, leo tena amefunga magoli mawili ya ushindi katika mchezo huo.

  
Benzema alianza kufunga goli la kwanza katika dakika ya 19, kabla ya Sabin kuisawazishia Athletic katika dakika ya 67, Benzema tena dakika tatu baadae akaiandikia Madrid goli ushindi.

  
Madrid sasa wanakaa kwenye uongozi wa La liga wakiwa na pointi 13 baada ya kucheza michezo mitano, wakifuatiwa na Celta Vigo.

  

Tupia Comments