Michezo

Fulltime ya Arsenal vs Tottenham hii hapa (Capital One)

on

Michuano ya kombe la ligi maarufu kama Capital One yameanza leo rasmi kwa viwanja kadhaa kuwaka moto nchini Uingereza.

  
Arsenal wakiwa nyumbani katika dimba la Emirates leo waliwakaribisha mahasimu wao wa jadi klabu ya Tottenham Hotspur.

Mchezo huo umemalizika kwa vijana wa Arsene Wenger kuibuka na ushindi mgumu w 2-1 dhidi ya vijana Pochettino.

  
Matheiu Flamini aliifungia Arsenal magoli yote mawili katika dakika ya 26 na 78 za mchezo huo, huku Chambers akijifunga katika dakika ya 56.

  
Hii ndio mechi ya kwanza kwa Flamini kufunga magoli mawili katika mechi moja tangu alipoanza kucheza soka la ushindani.

Tupia Comments