Michezo

Fulltime ya Man Utd vs Ipswich Town – wafungaji na pichaz

on

Wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa mapema na kwa aibu msimu uliopita kwenye michuano ya Capital One – wakifungwa na timu ndogo ya MK Dons, klabu ya Manchester United leo imejitupa uwanjani kukipiga dhidi ya Ipswich Town.

  
United leo wamefanikiwa kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya Ipswich katika mchezo uliochezwa katika dimba la Old Trafford.

  Baada ya ukame wa muda mrefu, nahodha wa United Wayne Rooney leo alianza kuifungia timu  yake goli la kwanza katika dakika ya 23 ya mchezo huo, goli lilodumu mpaka mapumziko.
  Kiungo kinda ya kibrazil Andres Pereirra akaifungia United kwa mkwaju wa faulo kipindi cha katika dakika ya dakika ya 60 ya mchezo.
  Na katika dakika ya 90+2 mshambuliaji mpya wa timu hiyo ya Manchester United Anthony Martial akaweka kimiani goli la tatu na kuiwezesha timu yake kwenda mbele katika hatua  ya raundi ya 4 ya Capital One.

Tupia Comments