Mkurugenzi wa lebo ya Freebandz, Future Hendrix maarufu kwa jina la kisanii, Future anazianika headlines za leo baada ya taarifa kusambaa kuwa alilipwa pesa ya kufanya show lakini kufikia siku ya show rapper huyo hakuonekana.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ wa Marekani, promoter mwenye jina Robert Caillier ameamua kupeleka issue yake mbele ya Mahakama na kwenye madai yake, promoter huyo anadai dola 150,000 mshiko ambao kwa pesa ya nyumbani unagusa mpaka milion 300!
Licha ya hayo promoter huyo anadai kuwa aliilipa management iliyokuwa inahusika na Future kwa ajili ya show hiyo deposit ya dola 15,000 (milion 30 za Tz) pesa ambayo pia anaomba arudishiwe.
Team ya Future haijakaa kimya, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na TMZ, inasemekana rapper huyo alikuja kwenye show hiyo na alipanda jukwaani kutoa show husika lakini baada ya muda walimshusha msanii wao baada ya kugundua kuwa Promoter wa show hiyo hakuwa na hela kamili ya Future.
Kwa show moja tu ya Future, rapper huyo hupokea mzigo wa dola 150,000 (milion 300 za Tz) na promoter huyo hakuwa na kiasi kamili cha pesa hiyo… kesi hiyo itasikilizwa Mahakamani kwa mara ya kwanza hivi karibuni.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.