Habari za Mastaa

Mengine ya Future kuhusu yeye na Ciara, Urafiki wake na Drake + Beef yake na Meek Mill!

on

Kumekuwa na maneno mengi sana baada ya rapper Future na msanii wa R&B Marekani Ciara kuachana… wengi walisema kosa lilikuwa la Future, na Future alipoulizwa alisema kuwa tatizo halikuwa lake bali mama wa mtoto wake Ciara ambaye alitaka kuharakisha ndoa kati yao kitu ambacho hakuwa tayari kufanya vile ambavyo Ciara alikuwa anataka.

fewtch2

Future & Ciara.

Maisha yakaendelea na Ciara akapata mpenzi mpya… maneno yakaanza upya baada ya mpenzi huyo, Russell Wilson kuanza kujenga ukaribu na mtoto wa Future na ikasemekana kuwa Future hakupenda kitendo cha Ciara kumkaribisha mwanaume huyo kwenye maisha ya mwanao akiwa bado mdogo sana… Sasa basi Future alipata time ya kufanya interview na kueleza kile anachokifiria kuhusu Ciara, mpenzi wake pamoja na mtoto wao…

>>>Mimi niko poa kabisa kwa Ciara kuwa na mtu yoyote anaependa kuwa nae, ila kuna mazingira ambayo kama baba siyapendi haswa kwa sisi ambao maisha yetu kila siku yapo kwenye lens ya camera… huwezi tu ukamuachia mwanaume yoyote atembee na mwanangu ajisikiavyo, sijui kama unanielewa? Nahisi vitu vingi anavyovifanya Ciara ni vya kiubinafsi, sijui ni roho mbaya au nini ila ni ubinafsi, natakiwa nishirikishwe kwenye kila kitu anachokifanya juu ya mwanangu lakini kutoa nafasi hiyo kwa mwanaume ambaye hajachangia damu yake, kwangu huo ni ubinafsi na dharau inabidi mimi pia niridhike ndio mengine yafuate!<<< Future.

fewtch3

Rapper Meek Mill.

Na alipoulizwa kuhusu beef yake na Meek Mill, Future alikuwa na haya ya kusema…

>>> “Kusema kweli nampenda Meek Mill, na uhusiano wangu na Drake nahisi uko poa tu, tumekuwa tukijenga urafiki mzuri sana kwa miaka michache sasa na ninamheshimu sana Drake na pia tumeshafanya tour kadhaa pamoja na kusema kweli napenda vibe yake, yupo real na ni mtu ambae anaweza akaniamini na mimi nikamuamini… uhusiano wangu na Drake umekuwa ukijijenga vizuri juu ya heshima tulionayo kwa kila mmoja na pia juu ya heshima ya kazi..!” <<< Future.

Future ameachia mixtape yake mpya na Drake ‘What A Time To Be Alive’ ambayo mauzo yake ya wiki ya kwanza yanategemea kufika idadi ya copy 500,000!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasamuziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments