Hali ya sintofahamu imetokea mjini Harare Zimbabwe leo asubuhi baada ya Jeshi la nchi hiyo kuzingira Ikulu na maeneo mbalimbali ya mji huo likiwa na zana za Kijeshi vikiwemo Vifaru na kusababisha wengi kupata uoga hata wa kutoka kwenda kazini
Inaelezwa kuwa Jeshi limekifunga kwa muda kituo cha Televisheni cha Taifa na kufunga mwingiliano na ofisi za serikali jambo ambalo Wananchi walilitafsiri kuwa yawezekana likawa jaribio la jeshi kupindua Serikali ya Robert Mugabe.
Baada ya taharuki hiyo Mkuu wa Jeshi Meja Jenerali SB Moyo amekanusha taarifa hizo na kusema Rais Robert Mugabe yuko salama IKULU na hakuna jaribio lolote la kupindua nchi.
Meja Jenerali Moyo ameeleza kuwa jeshi limefanya hivyo kwani linawasaka wahalifu ambao wamekua wakipanga mashambulizi dhidi ya Serikali na pindi tu watakapowakamata, hali itarudi kama kawaida.
ULIPITWA? TAZAMA MAKOMANDO WA TANZANIA WAKIONYESHA UWEZO WAO, PLAY HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: MAKOMANDO WA TANZANIA WAKIPAMBANA BILA BUNDUKI… TAZAMA HAPA CHINI