Top Stories

Good News: Uwezekano wa kuwepo chanjo ya Ebola

on

Wanasayansi wameeleza tumaini jipya baada ya uchunguzi wa hivi karibuni kuonesha uwezekano wa kufanikiwa kuwepo kwa chanjo mbili za ugonjwa wa Ebola ambazo zinaweza kumkinga mtu dhidi ya maambukizi hayo kwa muda wa mwaka mmoja.

Utafiti huo mpya ambao umechapishwa na jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia kwa kuwashirikisha wagonjwa 1,500 ambao walipewa chanjo hii na kisha kukingwa na virusi vya ugonjwa huo kwa mwaka mzima.

Matokeo hayo yameonesha matumaini ya kuwa chanjo hiyo inaweza kuja kutumika katika siku za usoni. Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015.

Ulipitwa na hii? Kama una mpango wa kulima mbogamboga, kuna hii ya kufahamu

Soma na hizi

Tupia Comments