Burudani

G Nako aachia Minitape yake “Kitimoto”

on

Msanii wa Bongofleva G-Nako au kwajina lingine G Warawara ni miongoni mwa marapawanaojua nini cha kuwapa mashabiki wao na kwamuda gani! Rapa huyu ambaye ni moja yawanoaunda kundi la Weusi mara zote huwa hafanyikazi mbovu, iwe ni ya kwake au ameshirikishwa.

Kwa kujali mashabiki wake kuelekea mwishoni mwamwaka 2021, G-Nako ameachia Minitape yake kali ambayo ameipa jina la ‘Kitimoto

Watu wengi wanaweza kushangaa jina la Minitapehii, lakini kimsingi G-Nako mwenye amemaanishaKiti chenye Moto yaani mtu huwezi kukaa kwenyekitu muda wote lazima usimame kutokana na ukaliwa ngoma zilizopo kwenye Minitape hii.

Ngoma zote ni ‘Club Bangers’. Kila ngoma inayosikiliza hutamani iishe na pia hutatami kurushangoma yoyote ile, Minitape hii inajumuisha ngoma 9 za moto zenye kolabo za wasanii mahiri.

Ngoma zilizomo kwenye Minitape hii ni pamoja naUnakaaje Chini‘, ‘Stimu‘ ‘Poison’ ft. Country Wizzy, ‘Shika Shila‘ ft. Young Lunya, ‘Acha Dharau‘, ‘Booty Goo’ ft. Spicy Meg & Petra, ‘Loko Loko‘, ‘Ooh Mama’ pamoja naKitoko‘.

Mkali huyo ambaye jina lake halisi ni George Mdemu, huu unakua ujio wake mpya baada ya miezitisa kupita bila ya kuachia kazi zake mwenyewekama solo artist tangu aachie wimbo wake wamwisho ambao niJiachieuliotoka Machi 4, 2021.

G-Nako ni miongoni mwa marapa wachacheTanzania ambao wamekuwa na unyumbulifu(flexibility) mkubwa katika sanaa ya muzikikutokana kujaaliwa uwezo wa kuimba pamoja na ku-rap.

Minitape hiyo inapatikana Boomplay kwa sasa naunaweza kuisikiliza kupitia link hapa chinihttps://www.boomplay.com/share/album/36325670

Soma na hizi

Tupia Comments