Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mke wake Neema Lema wamesomewa maelezo ya awali ya kusambaza ujumbe wa kuudhi kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo Wakili wa serikali Alice Mtenga Ameieleza mahakama kwamba wameaandaa mashahidi watano na watakuwa na vielelezo ikiwemo simu ya Mshtakiwa.
August 20 mwaka 2016 washtakiwa wote kwa kutumia simu ya mkononi waliandika ujumbe mfupi na kuutuma kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na msg yenyewe ilikua inasema ‘Karibu tutakudhibiti kama Arabuni wanavyodhibiti Mashoga‘
Mshtakiwa ambaye ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekana tarehe ya kukamatwa na kumtumia ujumbe huo wa kuudhi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo Wakili wa Lema, John Malya amesema wameweka pingamizi la maandishi kutokana na kuwepo kwa upungufu katika hati ya mashtaka
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo John Baro amehairisha kesi hadi February 3 ambapo pingamilizi hilo litasikilizwa lakini pia Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema amesomewa shtaka la kuhamasisha watu kufanya kusanyiko lisilokuwa na kibali kupitia mtandao wa kijamii
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Bernard Nganga amepanga kutolea uamuzi mdogo kuhusu hoja iliyoletwa na upande wa mshtakiwa kuhusu kesi hiyo kuhamishiwa katika mahakama ya kikatiba yenye majaji watatu, unaweza kutazama video fupi ya leo kwa kubonyeza play hapa chini
Mke wa mbunge wa Arusha mjini Neema Godbles lema ameongezwa kwenye kesi ya kutuma ujumbe wa kuudhi kwa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. pic.twitter.com/ux3UVvOBmy
— millard ayo (@millardayo) November 1, 2016
ULIPITWA? Baada ya Mbunge wa Kilombero kuhukumiwa miezi 6 jela, sheria inasemaje kuhusu kuupoteza Ubunge wake?