Burudani

Tweet ya Rapper Nick Minaj kutangaza kuacha muziki

on

NI headlines za Rapper wa kike kutokea Marekani, Onika Tanya Maraj maarufu kama Nick Minaj ambae leo Septemba 5, 2019 ameutangazia umma kustaafu kazi ya Muziki.

Staa huyo ameujulisha umma kustaafu kwake kupitia mtandao wake wa twitter kwa kuyasema haya’Nimeamua kustaafu niwe na familia yangu najua kwasasa mtakua na furaha, kwa mashabiki zangu endeleeni kushirikiana na mimi mpaka kifo changu’– Nick Minaj.

Baada ya Nick Minaj kuandika ujumbe huo mashabiki wamekuwa na maswali pasipo na majibu juu ya uamuzi huo uliofanywa na staa huyo.

Rekodi ya mwisho ambayo ilimrudisha kwenye headlines mnamo June 21, 2019 inaitwa Megatron ambayo kupitia mtandao wa  Youtube rekodi hiyo imetazamwa na zaidi ya watu 64,011,930

Soma na hizi

Tupia Comments