Top Stories

VIDEO: Inabidi Muielewe tu Taifa Stars, Msuva Kaongea Kwa Hisia

on

June 23 2019 ilikuwa ni siku ya kihistoria na masikitiko kwa Tanzania, kihistoria ni kutokana Tanzania imecheza game yake ya kwanza ya fainali za AFCON baada ya miaka 39 ya masikitiko kwa sababu imepoteza mchezo wake huo dhidi ya Senegal kwa magoli 2-0, leo kwenye mazoezi Simon Msuva amefunguka na kuelezea sababu za kufungwa kwao.

“Katika matokeo ya pili haya yanatokea unaweza ukashinda au ukafungwa, mchezo wetu wa kwanza wa jana tumepoteza kwakweli viwango vyao vipo juu siwezi kusema uongo, mbele yenu hapa leo naongea kama Simon tumecheza na watu wa viwango vya juu”>>> Simon Msuva

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mchezo ujao utachezwa dhidi ya timu ya taifa ya Kenya ambayo nayo imetoka kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria kwa magoli 2-0, kwani yoyote kati ya Kenya na Tanzania akipoteza mchezo huo ni wazi atakuwa ameaga mashindano hayo kwa asilimia kubwa au asubiri baraka za Best Looser.

VIDEO: Kutokea England hadi Cairo, Mzungu huyu shabiki damu wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments