Ad

Habari za Mastaa

Barua ya Mwanzilishi wa Facebook na mkewe waliyomwandikia mtoto wao

on

Ni kawaida kwa matajiri na watu maarufu duniani kuwawekea mipaka ya kucheza watoto wao na kuhakikisha wanaishi mazingira ambayo sio ya kuchangamana sana na jamii ukiachilia mbali sababu za kishule nia yao ikiwa ni kuwalinda na mambo mbalimbali.

Hii imekua tofauti kwa mwanzilishi wa Facebook Mark Zucherberg na Mkewe Priscilla Chan ambao wameamua kumwandikia barua ya upendo mtoto wao wa pili aliyezaliwa hivi karibuni aitwaye August wakimuusia kutumia muda wake wa utoto vizuri kwa kucheza nje na kufurahia utoto wake na watoto wengine kabla hajawa mtu mzima kwa kwa kuwa atakua busy sana.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka>>>”Utoto ni mzuri sana, na unapata nafasi ya kuwa mtoto mara moja tu maishani. Kwa hiyo, usiishi utoto wako kwa kuhofia jinsi kesho yako itakavyokuwa kwa sababu tuko hapa kwa ajili hiyo. Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa ulimwengu unakuwa sehemu bora ya wewe kuishi na watoto wote wa kizazi chako.”

ULIPITWA? Duka la mwimbaji Jux lapitiwa na bomoabomoa ya ghafla DSM…tazama hapa kwenye hii video!!!

ULIPITWA NA HII VIDEO ILIYOSAMBAA!!! Ni Harusi ya Diamond na Zari????? 

Soma na hizi

Tupia Comments