AyoTV

Haruna Niyonzima hatocheza dhidi ya KMC licha ya kuwasili na timu

on

Kocha Mkuu wa AS Kigali Eric Nshishimana aliongea na waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wao wa marudiano wa kuwania kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la shirikisho Afrika dhidi ya KMC, game hiyo itachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na matokeo ya kwanza Kigali yalikuwa sare ya 0-0, hivyo yoyote anaweza kupata matokeo na akasonga mbele, Nshiyimana ameeleza kuwa katika mchezo huo kikosi chake hakitakuwa na Haruna Niyonzima kutokana na kukosa vibali kutoka CAF.

Hata hivyo KMC nao wanachangamoto kama AS Kigali kwani kiuongo wao raia wa Rwanda Jean Mugiraneza hawezi kucheza pia kwa kukosa vibali kamili, KMC ili afusu anahitaji ushindi wa aina yoyote wakati AS Kigali atakuwa anahitaji sare ya magoli.

VIDEO: Kwa tathmini hii ya Edo Kumwembe, Mashabiki wa Chelsea haina budi kuwa wavumilivu

Soma na hizi

Tupia Comments