Shahidi wa upande wa mashtaka, Timos Emekea ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 28, 2017 kuwa hafahamu maana ya maneno ‘Dikteta Uchwara’ aliyoyasema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu katika kesi yake ya kutoa lugha ya uchochezi.
Aidha, Shahidi huyo ambaye ni watano, amesema alimsikia Lissu akitamka Rais Magufuli ni Rais uchwara na ni Rais dikteta ambaye Watanzania wasipokuwa makini wataingia kwenye Giza nene hawapaswi kumuunga mkono.
Akiongozwa na wakili wa serikali, Paul Kadushi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa ambapo shahidi huyo amedai>>>>”Baada ya kusikia maneno hayo, sikujisikia vizuri, kusikia rais anayetuongoza ni uchwara hivyo nikasogea pembeni si kuendelea kusikiliza.”
ULIPITWA? TUNDU LISSU: “Mawakili wasusie kwenda Mahakamani”