Nahodha wa timu ya FC Barcelona Lionel Messi anaamini kuwa mchezaji mwenzake wa zamani Neymar anaweza kujiunga na Real Madrid na sio kurudi FC Barcelona kama inavyoaminiwa na wengi.
Messi kupitia interview yake ya RCA 1 ya Hispnia aliyoifanya hivi karibuni inaeleza kuwa Messi anamini kuwa Rais wa Real Madrid Fiorentino Perez anaweza kufanya kitu ili kumshawishi ajiunge nao.
“Kwa dhati kabisa nafikiri kitu kimoja hususani katika soko la sasa, kama hatokuja hapa (Barcelona) atakwenda Madrid kwa sababu alitaka kuondoka (PSG) na alisema hivyo, nafikiria Florentino na Real Madrid watafanya kitu fulani ili kumchukua” >>>Messi