Michezo

PIGO: Serengeti Boys imepata pigo jingine ikiwa Gabon

on

Michuano ya AFCON U-17 hatua ya makundi kwa michezo ya kundi B ilichezwa katika uwanja wa Libreville Gabon ambapo game ya kwanza ilikua ni Tanzania vs Mali ambapo mpaka Full Time game iliisha kwa 0-0.

Wakati Serengeti Boys tayari ikiwa ina pigo jingine la Nahodha wake Issa Makamba kuondolewa kikosini kutokana na kupasuka mfupa huku Madaktari wakithibitisha kwamba atachukua miezi mitatu kupona, mwingine wa Serengeti Boys ameumia.

Ni Mshambuliaji Abdul Selemani ambaye ameumia kichwani na Madaktari wanasema atakuwa nje ya uwanja kwa siku saba kutokana na jeraha hilo la kichwani kwa nyuma lililosababisha pia kushonwa nyuzi nne, ni jeraha ambalo aligongana na mpinzani wake wakirukia mpira juu.

Kwenye hii video hapa chini Daktari wa timu ameongea na AyoTV na kusema ‘kitaalamu kwa kawaida tukishona kidonda kinakaa siku 7 na kisha kinaangaliwa kama ngozi imeunga, kama bado matibabu itabidi yaendelee’

VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera

Soma na hizi

Tupia Comments