Premier Bet SwahiliFlix Ad Halotel Ad

Michezo

Mtu wangu wa soka hii ni kwa ajili yako, tayari nchi itakayoandaa AFCON 2017 imetajwa..

on

foot-ball1Ghana, Algeria na Gabon zote ziliangusha karata ya bahati nasibu kwenye Shirikisho la Soka Afrika CAF ambapo kila moja ilijipa nafasi ya kushinda ili kuteuliwa kuandaa Michuano ya CAF mwaka 2017, tayari leo Dunia imejua nani kaibuka na ushindi kati yao.

Taarifa iliyotolea leo April 8 2015 kutoka Cairo, Misri ni kwamba Shirikisho hilo la soka Afrika CAF limetangaza kuwa Gabon imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Libya ndio nchi iliyokuwa iandae michuano hiyo lakini iliomba iondolewe kwenye nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama kuwa sio nzuri.

Shirikisho la soka Afrika CAF limeichagua Gabon ambayo ilikuwa ikigombea nafasi hiyo pamoja na Ghana pamoja na Algeria ambayo huenda imepoteza nafasi hiyo kutokana na hali ya usalama katika viwanja vyake baada ya tukio la kifo cha mchezaji wa Cameroon, Albert Ebosse mwaka 2014.

millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa….  unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Soma na hizi

Tupia Comments