Siku moja baada ya uchaguzi nchini Gabon, ukusanyaji wa matokeo kutoka majimbo mbalimali unaendelea, baada ya Uchaguzi Mkuu, Jumamosi Agosti 26, uliyojumuisha uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge na uchaguzi wa serikali za mitaa.
Siku ya Jumamosi, kulishuhudiwa hitilafu nyingi na zoezi la upigaji kura lilichelewa kuanza katika vituo vingi vya kupigia kura. Hali ya kisiasa imezidi kuwa tete siku ya Jumapili mchana.
Siku ya Jumamosi, mgombea mkuu wa upinzani, Albert Ondo Ossa aliishutumu serikali kwa udanganyifu na, mwisho wa siku, serikali ilitangaza kukata mara moja mtandao na sheria ya kutotoka nje kuania siku ya Jumapili hii jioni, saa moja kamili, hadi saa 12 kamili asubuhi.
Katikati ya alasiri ya Jumapili hii, Agosti 27, hali ilikuwa shwari.
Teksi na magari ya uchukuzi yalikuwa yakifanya kazi zao kama kawaida, watu waliokuwa kanisani walikwenda nyumbani. Hata hivyo, kulingana na shuhuda kadhaa, maafisa wengi wa polisi wameonekana katika maeneo mbalimali.
Vikosi vya usalama vimetumwa katika baadhi ya vituo vya mafuta. Katika njia panda ya Rio, inayojulikana sana kwa kuwa kitovu cha maandamano, magari mawili ya polisi ya kuzima fujo na zimamoto yameedeswa katikaeneo hilo.
Inatarajiwa kuwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi itaongezwa ifikapo jioni kabla ya kuanza kutekelezwa kwa sheria ya kutotoka nje saa moja kamili usiku.
Tayari siku ya Jumamosi jioni, vizuizi vya barabarani vilianza kuonekana katika baadhi ya maeneo.
Miongoni mwa wakazi, baadhi ya wakazi tulioongea nao hawafichi wasiwasi wao. Wanaogopa hasa kutangazwa kwa matokeo na mgogoro mpya wa baada ya uchaguzi.
Mnamo 2016, kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kulisababisha vurugu kubwa. Siku ya Ijumaa, ilikuwa siku ya malipo, wengi walienda madukani kununua vyakula visivyoharibika.
Mtandao wa nchi hiyo ulizimwa na mamlaka ilifanya baada ya uchaguzi na wanasema hii inapaswa kutumika kukomesha habari za uwongo na wito wa chuki.
Hata hivyo, kulingana na Gemal Affagnon, meneja wa shirika la Mtandao bila mipaka katika Afrika Magharibi, hatua hii inaonyesha kutokuwa na imani na uchaguzi.