Raia wa Gabon wanaitwa kushiriki kura ya maoni mnamo Novemba 16 kuhusu rasimu ya katiba mpya, hatua muhimu kuelekea kurejea kwa utawala wa kiraia ulioahidiwa na utawala wa kijeshi baada ya mapinduzi ya mwaka 2023, imetangaza serikali ya mpito.
Hatua ya mwisho ya utaratibu uliozinduliwa baada ya kutimuliwa kwa Rais Ali Bongo, rasimu ya sheria ya msingi ilipitishwa siku ya Alhamisi na Baraza la Mawaziri, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa jioni na Laurence Ndong, msemaji wa serikali inayoongozwa na Jenerali Brice Ngema Oligui.
“Baraza la Mawaziri lilionyesha kuridhishwa kwake na matokeo ya rasimu ya Katiba mpya .
Hatua inayofuata ya uamuzi katika mchakato wa mpito itakuwa ni kuandaa kura ya maoni ya katiba,” inabainisha taarifa hii kwa vyombo vya habari, huku ikisema kuwa sheria nne zimepitishwa ili kudhibiti utaratibu huo, mojawapo ikiitisha kura ya maoni “Novemba 16, 2024”, na nyingine inabainisha kuwa wapiga kura watakuwa na chaguo kati ya kura mbili, “Ndiyo” na “Hapana”