AyoTV

Kocha wa Simba baada ya kuwasili Zanzibar”Sio njia bora ya kuandaa timu”

on

Kikosi cha Simba SC leo Jumatano ya January 2 2019 kimewasili visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi Cup itakayofanyika mwanzoni mwa mwaka kila mwaka, Simba imewasili Zanzibar ikiwa na wachezaji 28 lakini Kocha wao Patrick Aussems amesema atatumia wachezaji wote kama sehemu ya kuwapumzisha na kuwapa nafasi na wengine.

Hata hivyo Ayo TV ilipomuuliza alipokuwa akiwasili kuwa michuano hii anaona ni njia sahihi kwake kuandaa timu tukiwa anaelekea kucheza game ya CAF Champions League alisema sio njia sahihi kwa upande wake zaidi ya kitu anachoona muhimu kwake ni timu tu kuwa pamoja ila anajua Mapinduzi Cup ina maana kubwa sana kwa Tanzania na Zanzibar kiasiasa.

“Kuhusu Mapinduzi Cup kiukweli kwangu ni kuwa pamoja katika mazingira tofauti na tutakiwa na uwezo wa kujiandaa na mchezo dhidi Js Saouro January 12 kwa bahati mbaya hatutocheza Mapinduzi Cup hadi mwisho kama tutaingia nusu fainali tutaleta team B kumalizia”>>>Patrick Aussems

“Ratiba zimeingiliana najua haiwezekani kuahirisha michuano ya Mapinduzi Cup na najua ni ngumu kuahirisha game ya Champions League, najua Mapinduzi Cup ni muhimu kwa Tanzania na Zanzibar kisiasa lakini pia SportPesa Super Cup inaingiliana hivyo hatuna jinsi lakini kiukweli hii michuano sio njia bora ya kuandaa timu vs Js Saouro”>>> Patrick Aussems 

VIDEO: Furaha ya ushindi Kocha wa Simba kashangilia hadi kavua shati

Soma na hizi

Tupia Comments