Michezo

Game ya Bayern na Atletico Madrid hati hati kuahirishwa

on

Imeripotiwa kuwa mchezo wa Kundi A kati ya FC Bayern Munich dhidi ya Atletico Madrid wa Ligi ya Mabingwa Ulaya leo unaweza kuahirishwa sababu ya winga wa FC Bayern Serge Gnabry kuthibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Wachezaji wa FC Bayern Much wote wamelazimika kufanyiwa vipimo tena katika round ya ziada kutokana na Serge Gnabry kuwa na maambukizi, hivyo wanahofia kuwa wanaweza kuambukiza wachezaji wengine.

Hadi sasa hayajatoka majibu ya moja kwa moja kama mchezo huo utachezwa au utaarishwa hadi majibu ya vipimo vipya vya wachezaji wa FC Bayern Munich yatoke.

Soma na hizi

Tupia Comments