Habari za Mastaa

The Game kaamua kuisogeza list yake ya rappers 10 wakali zaidi duniani, Eminem na Ice Cube watajwa!

on

Orodha ya The 10 Greatest Rappers of All Time ya Billboard inaendelea kuweka headlines tofauti kwenye mitandao ya kijamii… siku chache tu zilizopita tulishuhudia Snoop Dogg akisema kutokuwepo kwa 2 Pac kwenye orodha hiyo ni kitendo ambacho hakikuzingatia masharti na ubora wa muziki wa Hip Hop, Marekani.

Haikuishia hapo, kwa upande wa Bongo Flevani napo tulishuhudia msanii wa Bongo Fleva, Nikk wa Pili akiitoa list yake ya rappers 10 wakali wa Tanzaniana leo msanii wa HipHop kutoka Marekani, The Game ameona na yeye aisogeze list yake ya rappers 10 wakali zaidi…. watu walioguswa?!

bill4

Kupitia page yake ya Instagram, The Game alipost list yake na caption ya maneno iliyosema…

>>> “Billboard wanavuta bangi sio bure!!! Inabidi niwarekebishe maana huu ni uzembe na kosa kubwa kwa HipHop… na naomba mnielewe MSIRUDIE TENA KUFANYA KOSA LA NAMNA HII KWENYE ARDHI YA MUNGU, LA KUTENGENEZA LIST YA HIP HOP BILA KUMUWEKA 2PAC @SnoopDogg au @Icecube #F*BillboardList“<<< @losangelesconfidential.

bill

Baada ya kuandika caption hiyo, The Game akaiweka hewani list yake ya rappers 10 wakali zaidi duniani… na kuiita list hiyo ‘MY LIST’

10 Greatest Rappers Of All Time (Kwa mujibu wa The Game) ni….

1. 2pac & B.I.G
2. Nas
3. Rakim
4. Eminem
5. Jay-Z
6. Ice Cube
7. Snoop Dogg
8. Andre 3000
9. Jadakiss
10. Big L & F** YO OPINION !!!!!!!!!”

Je hapa vipi mtu wangu, unakubaliana na The Game? Au na yeye kuna watu muhimu kwenye game hajawagusia!?

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

 

Soma na hizi

Tupia Comments