Top Stories

Gari ya mgombea mwenza Urais CHADEMA yapata ajali Shinyanga

on

Gari anayotumia mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama  Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu imepata ajali eneo la Msoka Kata ya Ngogwa, Jimbo la Masalala mkoani Shinyanga, wakati wakitoka  kwenye mkutano wa Kampeni katika jimbo hilo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Afisa Habari wa CHADEMA Tumaini Makene kupitia ukurasa wake wa twitter amesema gari alilokuwa anatumia Mgombea Mwenza wa Urais CHADEMA imepata ajali na wote waliokuwa kwenye gari hiyo ni wazima wa afya.

“Tunamshukuru Mungu kwa kuwaponya katika ajali hii mbaya wote waliokuwa kwenye gari hii inayotumiwa na mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Salum Mwalimu Juma Mwalimu” Tumaini Makene

VIDEO FUPI: HELIKOPTA YA CCM IKIPITA UWANJANI TABORA

Soma na hizi

Tupia Comments