Familia za wanafunzi 142 kati ya 148 waliouawa katika shambulio la kigaidi la Al Shabaab kwenye Chuo cha Garissa Kenya wameruhusiwa kuchukua miili ya ndugu zao kwa ajili ya mazishi ambapo Serikali ililazimika kutumia mashine maalum kutambua baadhi ya miili ambayo iliharibika vibaya kutokana na majeraha ya risasi.
Hilo limeendelea lakini bado kuna ishu oinawaacha watu njia panda, zaidi ya wanafunzi 166 hawajulikani walipo, familia zao bado zimeendelea kulalamika kutokana na baadhi ya ndugu zao kutoonekana.
Uamuzi mwiingine mgumu uliotangazwa na Kenya ni kulitaka Shirika la Wakimbizi UNHCR ndani ya miezi mitatu kufunga kambi ya wakimbizi iliyoko mashariki mwa nchini hiyo pamoja na kuwarudisha kwao wakimbizi ambao ni raia wa Somalia zaidi ya laki nne.
Bonyeza play kusikiliza taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…
#RIP kwa ndugu zetu waliofariki kwenye shambulio hilo
millardayo.com ndio sehemu yako kuzipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook