Habari za Mastaa

Wema Sepetu aachiwa huru, Mwanasheria athibitisha

on

Mwanasheria Albert Msando ambaye ndiye alisimamia kesi nzima ya muigazaji Wema Sepetu kutokana na kosa la kusamabaza video pamoja na picha za ngono mwezi October na kudaiwa kuwa video hizo hazikuwa na maadili katika jamii.

Albert Msando kupitia ukurasa wake wa instagram ameweka wazi kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia shtaka hilo Wema Sepetu na kumuachia huru ambapo pia ameeleza adhabu ya kosa hilo kuwa ni faini siyopungua shilingi Milioni Thelathini au kifungo kisichopungua miaka 10 jela. 

“Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemfutia @wemasepetu shtaka la kusambaza video isiyo na maadili chini ya Kifungu 225(5) cha Sheria ya Uendeshaji Makosa ya Jinai na KUMUACHIA HURU. @wemasepetu alishtakiwa kwa kosa hilo Mwezi Novemba, 2018. Adhabu kwa kosa hilo ni faini isiyopungua Shilingi Milioni Thelathini au Kifungo kisichopungua miaka 10 jela au vyote”

“WITHOUT PREJUDICE: KILA MMOJA ANAPASWA KUJIFUNZA MATUMIZI BORA YA MITANDAO YA KIJAMII. Kutukana, kutumia lugha chafu, kudhalilisha, kukashifu, KUSAMBAZA picha zisizoruhusiwa nk ni makosa na ADHABU zake ni kali sana. Usichukulie poa. #TheDon” >>>Albert Msando

VIDEO: ANAEMSOMESHA MTOTO WA MASOGAGE AWAVAA MASTAA “ACHENI MIDOMO, STEVE KATOA HELA”

Soma na hizi

Tupia Comments