Leo September 30, 2016 Gavana wa Benki Kuu Tanzania Profesa Benno Ndulu ametoa taarifa ya hali ya ukuaji wa pato la taifa kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016 pamoja na hali ya madeni ya ndani na nje ambayo serikali imeanza kuyalipa kwa kutumia fedha za ndani.
Gavana Ndulu amesema serikali imeanza kupunguza madeni ya serikali kwa fedha za ndani kwa kiasi kikubwa mpaka kufikia shilingi bilioni 95 kwenye deni la taifa huku ikianza kujitegemea kwenye matumizi yake kwa fedha za bajeti yake bila kutegemea misaada ya wafadhili kutoka nje.
Aidha ameongeza kwamba serikali inatarajia kukusanya mapato makubwa zaidi mwaka huu kuliko kipindi kingine kilichopita na kueleza ukuaji wa uchumi wa taifa umekua kutoka asilimia 5.8 mwaka 2015 mpaka kufikia asilimia 7.9 mwaka 2016.
ULIMISS TAARIFA YA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MANUNUZI YA UMMA PPRA KUHUSU TAASISI ZA SERIKALI ZENYE VIASHIRIA VYA RUSHWA?