Habari za Mastaa

Jux -‘Vanessa ndio aliamua tuachane, sijawahi kuongea wala kuonana nae’

on

Leo August 2,2019 mwimbaji Juma Jux amefanya mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM na amefunguka vitu vingi ikiwemo sababu ya kuachana na Vanessa Mdee pamoja na mahusiano yake mapya na mwanadada kutokea Thailand Naika.

Jux amefunguka pia ikiwemo ishu nzima ya Vanessa Mdee kuamua kuwa-unfollow marafiki zake wa karibu na ametoa mtazamo wake kuhusu hilo na kusema hadhani kama ni kitu kizuri Vee alichofanya kutokana na walimpokea vizuri kipindi alipoanzisha mahusiano nae.

“Watu wamekuwa wakiongea juu ya sehemu ambazo nimekuwa nikienda na Naika na wanasahau kuwa hata Vanessa Mdee pia nilishawahi kwenda naye sehemu nyingi tu, Simpost mpenzi wangu kwa sababu ya ‘Kiki’ bali nikiona nimepiga picha na mwenza wangu why nisipost wakati tumetokea vizuri, mimi sio mtu muhuni yani nikiwa kwenye mahusiano huwa nayaweka wazi”

 “Sina sababu ya kuwa single na kwanini niwe single na sababu zipi za kufanya niwe single, nilishawahi kukaa muda mrefu bila mahusiano mara ya kwanza nilipoachana na Vanessa Mdee na ilikuwa miezi nane nilikaa hivyo sababu mimi ndiyo nilikuwa na kosa. Niliamua kuweka mahusiano yangu wazi baada ya yeye kuona anasema kuwa tumeachana hivyo nikaona haina haja ya kuficha mahusiano yangu na Naika”

“Kwenye mahusiano kuna wakati mapenzi yanaisha na kubaki mazoea hivyo Vanessa Mdee yeye ndiyo aliniambia kuwa anaona mahusiano yetu hayaeleweki hivyo akaomba tuachane, kiukweli iliniumiza sana na hata nilivyomuuliza sababu alinipa sababu ambazo siwezi kuziweka hadharani ila ni sababu ambazo unatakiwa uzielewe na kweli nilimuelewa”

“Sijui kwanini ameamua ku- unfollow watu wangu wa karibu wote na sidhani kama ni sawa kwani kama ingekuwa kila mtu ambaye unaachana naye una- unfollow watu zake wa karibu ingekuwa mbaya zaidi, akumbuke pia hata yeye wakati naanza naye watu wangu wa karibu walimpokea vizuri licha ya mtu ambaye nilikuwa naye kwenye mahusiano kipindi kile kupata matatizo”

Jux na mpenzi wake wa sasa, Naika

VIDEO: ‘MAADILI YA TANZANIA SIO KUTEMBEA UCHI” TAMKO LA BASATA KWA WASIMAMIZI WA MASHINDANO.

 

Soma na hizi

Tupia Comments