Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema siku ya Jumatatu kwamba Gaza inakuwa “kaburi la watoto”, na kuongeza matakwa ya kusitishwa kwa mapigano katika eneo hilo. Israel na wapiganaji wa Hamas wanaodhibiti Gaza wamepinga shinikizo la kimataifa la kusitisha mapigano.
Israel inasema mateka waliochukuliwa na Hamas wakati wa uvamizi wake kusini mwa Israeli mnamo Oktoba 7 wanapaswa kuachiliwa kwanza; Hamas inasema haitawaachia huru au kuacha mapigano huku Gaza ikishambuliwa.
“Operesheni za chini kwa chini za Jeshi la Ulinzi la Israeli na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu yanawakumba raia, hospitali, kambi za wakimbizi, misikiti, makanisa na vituo vya Umoja wa Mataifa – ikiwa ni pamoja na makazi.
Hakuna aliye salama,” Guterres aliwaambia waandishi wa habari.