Yahya Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka 22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua nafasi.
Kupitia Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU zilisema baada ya kuachia madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi hiyo ndani ya siku 3 ila media nyingine zinasema amepewa saa tu za kuondoka.
TV ya habari Nigeria imesema ECOWAS walimpa hadi saa sita mchana kuondoka lakini mwenyewe akaomba muda huo usogezwe hadi saa kumi jioni na imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.
Barrow aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya Gambia leo’
Sheria inasemaje kwa Rais kuapishiwa nje ya nchi kama ilivyotokea kwa mshindi wa Gambia? bonyeza play hapa chini