Michezo

UEFA imetangaza viwanja vitakavyochezewa fainali ya Champions League

on

Shirikisho la soka Ulaya UEFA leo limetangaza viwanja vitakavyotumika kuwa mwenyeji wa michezo kadhaa ya fainali ya UEFA Champions League kwa misimu kadhaa ikiwemo msimu wa 2020/2021, UEFA wametangaza viwanja mwenyeji wa fainali tatu zijazo za UEFA Champions League.

UEFA wametangaza kuwa msimu wa 2019/2020 mchezo wa fainali ya UEFA Champions League utachezwa Atatürk Olimpiyat Stadı nchini Uturuki katika mji wa Istanbul, wakati msimu unaofuatia wa 2020/2021 mchezo ho utachezwa katika uwanja wa St Petersburg.

Hayo yametangazwa katika mkutano wa kamati ya UEFA uliyofanyika Slovenia, huku ikitajwa kuwa maamuzi hayo yameangalia vitu vingi ikiwemo hoteli, miundombinu kwa maana ya ufikaji wa mashabiki kirahisi, mwaka 2022 itachezwa Allianz Arena nchini Ujerumani na 2023 utachezwa Wembley London England, hata hivyo UEFA pia wametaja jina michuano ya tatu ya vilabu Ulaya itakayoanzishwa itaitwa UEFA Conference.

VIDEO: Antonio Nugaz kaanza na Mbwembwe Yanga “Yanga unyonge kwisha”

Soma na hizi

Tupia Comments