Mix

Video: RC Makonda alivyomtembelea Hamisi Muhimbili DSM, ampa pesa za matumizi

on

Hamisi ni mtoto mwenye umri wa miaka 19 ambae amekuwa akijiuguza kwa muda mrefu kutokana na hali ya miguu yake kuvimba yote miwili.

Leo Machi 15, 2019 RC Makonda amemtembelea mtoto Hamisi aliyelazwa katika hospital ya Muhimbili DSM akiwa anapatiwa matibabu kutokana na tatizo lake la kuvimba miguu ambapo RC Makonda amemkabidhi mtoto Hamisi Laki Tano kwa ajili ya chakula huku akiahidi kuendelea kumpa msaada mpaka atakapo pona.

Pia Dkt Ibrahim Mkoma ambae ni mkuu wa Upasuaji kutoka Hospitalini hapo amethibitisha kuwa wameshabaini kinachomsumbua mtoto Hamis na wanaendelea na vipimo vingine kuangalia ni namna gani watahakikisha Hamisi anapona

 

Soma na hizi

Tupia Comments