Baada ya golikipa Juma Kaseja kufanikiwa kuipatia Taif Stars ushindi wa penati 3-0 na kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Juma Kaseja ndio alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kucheza penati ya kwanza iliyoleta nguvu kwa Taifa Stars na kuwadhoofisha Burundi, kiasi cha RC Makonda kumtangazia zawadi nono.
RC Paul Makonda leo hii ametimiza ahadi yake ya kumpa zawadi ya Tsh Milioni 10 golikipa Juma Kaseja baada ya kumtangaza kama nyota wake wa mchezo wa jana kati ya Tanzania dhidi ya Burundi, game hiyo iliisha kwa Tanzania kushinda kwa penati 3-0.
Tanzania ilicheza game hiyo na dakika 120 kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 1-1, goli la Tanzania likifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30 huku la Burundi likifungwa na Feiston dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, mikwaju ya penati ndio iliamua timu ipi isonge mbelee baada ya kuwa na aggregate ya 2-2.
VIDEO: Kaseja kashindikana kwa penati, cheki alivyodaka penati