Top Stories

Staa wa filamu Salman Khan kufungwa jela kwa ujangili

on

Mahakama nchini India imemkuta na hatia mwigizaji wa filamu za Bollywood, Salman Khan ya ujangili wa aina adimu ya swala mwaka 1998.

Khan anadaiwa kuua swala wawili wa aina ya ‘blackbucks‘ ambayo hulindwa sana nchini humo. Alifanya kosa hilo katika mji wa Rajasthan wakati wakitengeneza filamu.

Kutokana na hatua hiyo Khan anaweza kufungwa kati ya mwaka mmoja hadi sita jela lakini ana haki ya kukata rufaa. Waigizaji wengine wanne ambao waliigiza kwenye filamu hiyo pia walishtakiwa kwa kosa hilo.

Khan ambaye ana miaka 52, ni mwigizaji maarufu na wakongwe wa tasnia ya filamu India ambaye ameigiza filamu zaidi ya 100.

Zitto Kabwe kumpeleka Abdul Nondo Uhamiaji

 

Soma na hizi

Tupia Comments