Top Stories

Baada ya Polisi Geita kupigiwa simu kujua kilichosababisha wamshikilie Lowassa

on

Kutoka Geita Kanda ya ziwa jioni ya January 16 2017 zimetoka taarifa za mwanasiasa Edward Lowassa kushikiliwa na Polisi baada ya kuingia kwenye mkoa huo.

Kamanda wa Polisi Geita baada ya kupigiwa simu na millardayo.com na AyoTV amesema ‘ni kweli ameshikiliwa lakini nipeni muda kidogo kama baada ya saa moja niliweke vizuri kisha ndio niwape taarifa kamili, sasa hivi msiandike chochote mpaka nikamilishe

Wakati tukisubiria watachosema Polisi, chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kimetoa taarifa inayosema ‘Polisi wameshamchelewesha Mh. Lowassa kwenda kwenye mkutano wa kampeni kata ya NKOME , hii ndio inajionyesha ilikuwa dhamira yao

Kwenye taarifa yao CHADEMA walieleza zaidi kwamba sababu za kushikiliwa kwa Edward Lowassa hazikutolewa wala kosa alilolifanya halikutajwa baada ya kumuweka mikononi mwao, millardayo.com na AyoTV zinaendelea kufatilia na taarifa zote utazipata pindi zitakapotoka.

ULIPITWA? Tazama hapa chini kwenye hii video Askari Magereza walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Waziri wa mambo ya ndani

Soma na hizi

Tupia Comments