Mix

Kuhusu Mtanzania aliyepigwa na Mchina Geita mpaka kulazwa Hospitali

on

AzamTV News wameripoti kuhusu Raia wa China anayedaiwa kumpiga na kumjeruhi kwa kiwango kiasi kikubwa Mtanzania huko Geita mpaka kupelekea Mtanzania huyo kulazwa Hospitali.

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi amekiri kupokea malalamiko ya kijana huyo aliyelazwa kwenye Hospitali ya mkoa wa Geita baada ya kudai kupigwa ngumi na mateke sehemu za siri, kichwani, kiunoni na kifuani.

Daktari amesema sasa hivi Mgonjwa amepata nguvu ambapo walimuwekea mpira wa mkojo lakini kwa sasa wameutoa na anaweza kwenda chooni kama kawaida ambapo Mchina wa mgodi huo wa RD amesema hamna aliyepigwa.

Mwanasheria wa kampuni hiyo ya RZ Gold Mine amesemaNimepigiwa simu nyingi sana, wanatengeneza mazingira hayo wanapiga simu wanasema Mwambie Mchina asipotoa Milioni 2 nailipua, nimepigiwa simu mara mbili mara tatu naomba milioni mbili, naomba milioni mbili……… tumechoka sasa

Taarifa yenyewe ndio hii hapa chini kwenye video, bonyeza play kuitazama….

Soma na hizi

Tupia Comments