Muigizaji Jacquline Wolper ni miongoni mwa mastaa waliochukua headlines kwa mwaka 2017 kutokana na kuwa katika uhusiano na Harmonize na baadae kuachana na kuingia kwenye uhusiano mpya na mwanaume mwingine aliyekuwa akijulikana kama Brown.
December ya 29 ,2017 ameamua kutuonyesha kuwa mambo yameiva tayari ambapo anakaribia kuvishwa pete ya uchumba kutokana na posts alizozipost kupitia page yake ya instagram.
“unanishahurije baba kwenye engagement nivae kiutamaduni zaidi au english style ?usisahau pia nimesha fanya booking ya viti vya ukumbini vya sendoff pale ofisini kwenu ….nipo so excited na mwenye furaha for my special day ???”
Na post nyingine akaamua kuandika “kwaheri kwa Jacquline wa zamani”
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Jacquline Wolper kutangaza kuwa atolewa kwasababu mwaka 2015 alitangaza kuolewa na aliyekuwa mchumba yake na wengi walimfahamu kwa jina la Mkongo, je safari hii ataolewa kweli??? ingawa hajaweka wazi ni mwanaume gani atamuoa.
AUDIO:Mama Diamond hayajampita ya Hamisa na Zari