Michezo

Samatta amedhamiria kununua Private Jet?

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana Samatta baada ya kuichezea Taifa Stars game ya kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Uganda na game kumalizika kwa sare tasa (0-0), tayari amerejea katika club yake ya KRC Genk nchini Ubelgiji.

Samatta amerejea Ubelgiji na leo amepiga picha akiwa nje ya Jet ya KRC Genk na kuandika maneo yanayoashiria kuwa kwa sasa anatamani kumiliki ndege yake binafsi kama ilivyo kwa baadhi ya mastaa wa soka wa ulaya.

ndoto za kumiliki private jet zimeanza baada ya kupiga picha hii 🤨 sio kila ndoto inaweza kutimia ila, acha vita ianze😡” gharama ya chini ya private jet ni dola milioni mbili ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 4.4.

Kama ndoto ya Mbwana Samatta ya kutamani kumiliki Private Jet ikitimia atakuwa anaingia kwenye headlines moja na mastaa wa soka Cristiano Ronaldo wa Juventus, Gareth Bale wa Real Madrid, Neymar wa PSG na Lionel Messi wa FC Barcelona ambao nao wanamiliki Private Jet zao.

EXCLUSIVE: Licha ya kuwa na pesa na ustaa, hii ndio Sababu inayomfanya Samatta asiringe

Soma na hizi

Tupia Comments