Hivi karibuni Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limeeleza kuwa uchafuzi wa hewa yaani ‘air pollution’ kwa sasa ndilo tishio kubwa kwa afya duniani kote zaidi ya maradhi ya Virusi vya Ukimwi na Ebola.
Imeelezwa kuwa kwa sasa moja kati ya vifo vinne vya watoto wa miaka mitano vinatokana na athari za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na suala hilo la uchafuzi wa hewa na maji yenye takataka za sumu ambayo husababisha magonjwa.
WHO pia imetaja mji wa kwanza duniani wenye uchafuzi mkubwa wa hewa duniani kuwa ni Zabol nchini Iran ambapo uchafuzi huo ni mara ishirini zaidi ya kiwango ambacho kinakubalika na kushauriwa kwa siku ikifuatiwa na Gwalior na Allahabad nchini India.
Uliikosa hii? Naibu Waziri Mpina asimamia Viwanda viwili vikiandikiwa faini DSM