AyoTV

Kocha wa Serengeti Boys kaomba radhi, vipi kuhusu kujiuzulu?

on

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania U-17 leo imecheza game yake ya mwisho ya hatua ya Makundi ya michuano ya AFCON U-17 dhidi ya timu ya taifa ya Angola, Tanazania ilikuwa Kundi A lenye timu za Angola, Nigeria na Uganda,

Mchezo wa leo kwa Tanzania ulikuwa kama wa kukamilisha ratiba lakini wamejikuta wakipokea kipigo cha tatu mfululizo wakiwa wamefungwa jumla ya magoli 12 na kufunga 6 katika game zao za Makundi, kipigo cha leo cha 4-2 kutoka kwa Angola ndio kimewakwaza watanzania wote kiasi cha kuona kama fedhea kwa kuwa mwenyeji wa mashindano na kupoteza mechi zote.

Baada ya mchezo huo wakati mgumu ulikuwa kwa kocha wa Tanzania Oscar Mirambo ambaye aliombwa kutaka kujulikana msimamo wake “Tunaomba kutumia nafasi hii kuwaomba msamaha watanzania ambao walikuwa na matarajio makubwa kwa vijana wao sisi kama benchi la ufundi, tulijua tumefanya maandalizi ya kutosha”

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments