Top Stories

Inasikitisha: Kilichowapata watalii vikongwe Joberg

on

Kikundi cha watalii 36 kutoka Uholanzi nchini Afrika Kusini hivi karibuni wamevamiwa na watu wanaosemekana kuwa majambazi na kuwapora karibu mali zao zote pindi tu walipotua kwenye uwanja wa ndege wa Johannesburg nchini humo huku wakielekea hotelini.

Imeripotiwa kuwa watalii hao ambao karibu wote walikua ni wazee basi walilokua wamepanda lilisimamishwa na mtu aliyekuwa amevaa nguo za kiaskari akiwa na wenzake watano waliovaa kiraia na ndipo uhalifu huo ulipotendeka.

Watalii hao ambao walitembelea Afrika Kusini kwa lengo ka kukaa wiki tatu wameamua kurejea nchini kwao Uholanzi kutokana na tukio hilo lililowapata.

Ulipitwa na hii? “Walitishia kutupiga risasi wakachukuwa ng’ombe wetu” – Wanakijiji

 

Soma na hizi

Tupia Comments