Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo January 8, 2108 imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi December 2017 umepungua hadi kufikia 4% ikilinganishwa na 4.4% ilivyokuwa November 2017.
Kwa mujibu wa NBS hii inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa December 2017, imepungua ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwezi November 2017.
Kupungua kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula kufikia December 2017, ukilinganisha na bei za bidhaa kwa mwezi December 2016.
Baadhi ya vyakula vilivyosaidia kushuka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa mhogo kwa asilimia 1.9, nyama asilimia 3.4, samaki asilimia 15.1, karanga kwa asilimia 3.5, mbogamboga asilimia 2.9, njegere asilimia 7.5 na vinginevyo.
BREAKING: Msemaji Mkuu wa Serikali anazungumza na waandishi
Fedha zilizokusanywa na TRA kwa nusu ya Mwaka wa Fedha 2017/18