Habari za Mastaa

Ndani ya miezi 19 ‘Fall’ ya Davido yazidi kuwachanganya Wamarekani

on

Kwa mujibu wa mtandao wa Rolling stone Marekani unataja kuwa wimbo wa Davido ‘Fall’ umepata mzungumzko mkubwa kwenye maskio ya wananchi nchini humo  tokea uachiwe June 2,2017.

Pia kwa mujibu wa Nielsen wimbo huo unatajwa kuchezwa mara 482 hadi sasa kwenye radio 36 huku vituo vingine vinne vikitajwa kuongezeka wiki kadhaa zilizopita. Kwenye upande wa kusikilizwa Fall imeingia kwenye nyimbo 100 zilizosikilizwa zaidi Marekani kwenye Shazam na pia imeingia kwenye rekodi ya top 10 ya Shazam.

Midundo ya Afrobeats ya wasanii kama Mr Eazi imefanikiwa kupenya na kusikilizwa nchini Marekani kwa muda mfupi huku ikielezwa kuwa kwa msanii kuweza kupenya kwenye soko la Marekani hasa wimbo wake kusikika kwenye vituo vya radio itamgharimu kulipa shillingi laki mbili mpaka laki nne za Kitanzania ila Davido haijajulikana kama kalipa au hajalipa.

ARISTOTE: MASTAA WATANO WANAOVAA NYWELE ZA GHARAMA BONGO

Soma na hizi

Tupia Comments