Michezo

Boateng anaenda kuwaongezea nguvu Messi na Suarez ndani ya FC Barcelona

on

Kiungo wa kimataifa wa Ghana mwenye asili ya Ujerumani Kelvin Prince Boateng leo January 21 2019 ametangaza rasmi kuwa anaenda kujiunga na club ya FC Barcelona ya Hispania akitokea club ya Sassuolo ya Italia.

Boateng mwenye umri wa miaka 31 aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Tottenham Hotspurs, AC Milan na Schalke 04 atajiunga na FC Barcelona akitokea Sassuolo ya Italia kwa mkataba wa miezi sita na tayari Barcelona wamefikia makubaliano na mchezaji huyo.

FC Barcelona inamchukua Boateng kwa mkopo lakini wenye kipengele cha kumnunua wakivutiwa nae kwa euro milioni 8, hata hivyo baadhi ya watu wamekuwa na mashaka na Boateng kupitia account zao za twitter na wamehoji Barcelona wanataka Ubingwa au wanahangahikia kutoshuka daraja, Boateng amefunga magoli 57 pamoja na matano aliyoyafunga msimu huu akicheza game 15.

VIDEO: Mwalimu Kashasha kuhusu pasi ya Ajibu kwa Fei Toto “Locomotive faint”

Soma na hizi

Tupia Comments